HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 4, 2016

KAMATI ZA MAAFA ZATAKIWA KUFANYA TATHIMINI ZENYE UHALISIA.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya Monduli, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Francis Nyamiti akiongoza kikao cha kamati hiyo kujadili urejeshaji hali katika shule ya sekondari Edward Lowasa iliyopata maafa ya moto,, (wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya, tarehe 4 Februari, 2016. 
 Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya, (wakwanza kushoto) pamoja na wajumbe wa Kamati ya maafa wilaya Monduli wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Francis Nyamiti (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kamati hiyo kujadili urejeshaji hali katika shule ya sekondari Edward Lowasa iliyopata maafa ya moto tarehe 4 Februari, 2016. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Wilaya ya Monduli, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Francis Nyamiti (Mbele wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kikao cha kamati hiyo kujadili urejeshaji hali katika shule ya sekondari Edward Lowasa iliyopata maafa ya moto, (Mbele wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya, tarehe 4 Februari, 2016. 
(Picha zote na Ofsi ya Waziri Mkuu).

Na. Mwandishi maalum.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa imezitaka Kamati za Maafa za Mikoa, Wilaya na Vijiji zote nchini kufanya tathmini zenye uhalisia wa athari za maafa yanapotokea wakati wanapokuwa wanatekeleza jukumu hilo ambalo husaidia kuainisha hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika Kuzuia/Kupunguza, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali baada ya maafa kutokea. 

Akiongea wakati alipokutana na Kamati ya maafa ya Wilaya ya Monduli Tarehe 4 Februari 2016, Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa inapokea maombi ya misaada ya maafa ambayo tathmini zake huwa zimefanywa na Kamati za maafa ikiwa na aidha thamani kubwa au idadi kubwa kulingana na hali halisi ya athari ya maafa. 

“Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya uratibu maafa inalojukumu la kuratibu shughuli za maafa katika hali ya kujiandaa, kuzuia, kukabili na kurudisha hali ya kawaida pindi maafa yanapotokea. Katika ngazi ya wilaya maafa yakiwashinda kuyakabili huomba msaada katika ngazi ya mkoa halikadhalika mkoa ukishindwa huomba msaada katika ngazi ya kitaifa. Mfano mzuri ni maombi ya chakula cha msaada tumekuwa tunapokea maombi ya maefu ya tani lakini wataalamu wetu wakifanya tathmini ya kujiridhisha maombi hayo huwa mamia ya tani na wananchi huridhika” amesema Brig. Jen. Msuya 

Msuya aliongeza kuwa kamati hazinabudi kuelewa kuwa nchi yetu inakumbwa na majanaga ya asili na yale ambayo husababishwa na wanadamu ambapo kimsingi serikali inalojukumu la kuzuia au kupunguza athari za maafa hayo. Hivyo uongezaji wa thamani na idadi ya mahitaji ya misaada ya maafa hufanya waathirika wengine kutopata misaada kwa wakati pamoja na iliyopungufu kwa kuwa serikali huanza kutafuta rasilimali za ziada ili kuweza kukabili na kurejesha hali ya maafa husika. 

“Kamati ya maafa ya wilaya hii imefanya tathimini kwa uhalisia kwa maafa ya moto yaliyotokea shule ya sekondari ya Edward Lowasa, uhalisia wa tathimini hii umewezesha Kamati ya wilaya kuweza kumudu kurejesha hali ya shule hii kwa kuwa hakuna uongezaji wa thamani wala idadi. Tukifanya hivi kwa kamati zote nchini katika ngazi zote tutaweza kuwa na menejimenti nzuri ya maafa nchini”, alisisitiza Brig. Jen. Msuya. 

Awali akiongea katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Monduli Franicis Nyamiti alifafanua kuwa mara baaada ya maafa ya moto kutokea katika shule ya sekondari Edward Lowasa, kamati ya maafa imekutana ili kuweza kujadili urejeshaji hali wa shule hiyo ambapo taarifa ya tathimini ya athari ya maafa iliyofanywa na Kamati ya Wilaya ndiyo iliyokuwa inawaongoza katika utekelezaji. 

“Ni dhahiri kuwa taarifa ya tathimini ikiwa na uhalisia mara nyingi idadi na thamani mnaweza kuimudu kwa kushirikiana na wadau wa maafa. Sisi tumewashirikisha wadau hao ambao tayariwamejitokeza kutupatia magodoro yote 72 yaliyoungua, mansanduku ya wanafunzi hao pamoja na mchanga wa ujenzi. .”alisisitiza Nyamiti.

Nyamiti alifafanua kuwa uhalisia wa tathmini ya athari za maafa hufanya urejeshaji hali kuwa kwa wakati kwani tayari mdau mwingine amaeshajitolea kubomoa mabaki ya jingo la bweni lililoungua tayari kwa kuanza ujenzi, aidha Mmiliki wa shule jirani ya Tumaini sekondari amejitolea bweni lake, vitanda na magondoro amabavyo wanafunzi hao watakuwa wanatumia wakati ujenzi ukikamilika.




Shule ya Sekondari ya Edward Lowasa inao wanafunzi 700 ambapo wanafunzi 72 ndio walioathirika na maafa ya moto yaliyotokea tarehe 27 Januari, 2016 kwa kuungua bweni la wanafunzi hao. Aidha kutokana na maafa hayo hakuna mwanafunzi aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa . 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad