Na Nyakongo Manyama
Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Mkoani Mara imesema imepata ufumbuzi wa changamoto ya wanafunzi wa darasa la kwanza na awali Shule ya Msingi Mwibagi wilayani waliokosa mahali pa kusomea kwa kuwagawa wanafunzi hao kwa awamu mbili.
Hayo yamebainishwa leo (Alhamisi 04, Februari 2016), Afisa Elimu wa Wilaya hiyo, Hans Mgaya, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii, ambapo alikiri kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa madarasa shuleni kutokana na ongezeko la wanafanuzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza mwaka huu, ambapo hata hivyo tayari wameshachukua hatua mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo.
Aidha, Mgaya amesema kuwa jitihada za muda mfupi walizozifanya ni kuwagawa wanafunzi hao katika mikondo miwili ili waweze kubadilishana madarasa , mkondo mmoja utaingia asubuhi na mkondo mwingine mchana.
Kwa mujibu wa Mgaya alisema jitihada za muda mrefu ni kujenga shule nyingine mpya ili kusaidia kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja, ujenzi wa shule hiyo ulishaanza kabla ya tamko la elimu bure na tupo katika hatua ya awali ya ujenzi wa msingi wa madarasa hayo alisema Mgaya.
“wanafunzi walioandikishwa kujiunga na shule ya msingi kwa mwaka huu 2016 imeongezeka kwa kiasi kikubwa hivyo kusababisha idadi ya wanafunzi kuwa kubwa” alisema Mgaya.
Idadi ya wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza walioandikishwa kwa mwaka 2016 katika shule ya msingi Butiama kuanza masomo, ambapo hata hivyo zaidi ya wanafunzi 240 wa shule hiyo wanasomea katika chumba kimoja.
No comments:
Post a Comment