HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 4, 2016

BONNY MWAITEGE WAKWANZA TAMASHA LA PASAKA 2016.

Na Mwandishi Wetu.
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, Bonny Mwaitege (Pichani)amekuwa wakwanza kuthibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 27 jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama kamati yake inaendelea na mchakato wa maandalizi huku wakifuatilia maombi ya mikoa mingine ambayo ina dhamira ya kufikiwa na Tamasha la Pasaka.

“Bonny Mwaitege ni mwimbaji wa kwanza kuthibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka 2016 ambalo tumepanga kufanyika Mwanza, tumeridhika na maombi ya wakazi wa Mwanza ambao idadi kubwa ya maombi yao imeleta msukumo kwa Kamati yangu kushawishika,” alisema Msama.

Msama alisema wanaendelea na mchakato wa mazungumzo na waimbaji wengine wa muziki wa Injili ambao watapanda jukwaani katika Tamasha la Pasaka.

Naye Mwaitege alisema Mungu ni wa kushukuriwa kwa sababu ni jambo jema ambalo linanipa faraja ya kumtumikia kupitia nyimbo za injili.

Mwaitege alitumia fursa hiyo kuipongeza Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka kwa kumpa nafasi ya kwanza kuthibitisha kushiriki tamasha hilo.


Aidha Mwaitege alitoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo lina dhamira ya kusaidia jamii yenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad