Meneja wa kitengo cha Airtel Money, Asupya Naligingwa akiongea na waandishi wahabari ( hawapo pichani) wakati wakutangaza kutoa gawio la faida kwa wateja wa Airtel Money na Mawakala wake nchi nzima
· zaidi ya shilingi bilioni 3 kutolewa kwa wateja nchi nzima
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kutoa gawio la faida kwa wateja wake wa Airtel Money zaidi ya milioni 6 pamoja na mawakala wake nchi nzima.
Airtel italipa gawio la faida iliyopatikana kwa watumiaji wa huduma ya Airtel money kwa kipindi cha kuanzia Aprili 2015 hadi Desemba 2015 , ambapo kila mteja wa Airtel Money atapokea gawio lake kulingana na kiasi cha salio lake katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku
Akiongea na waandishi wa habari, Meneja wa kitengo cha Airtel Money “Asupya Naligingwa alisema” Tunayofuraha kubwa kutangaza mpango wetu wa kugawa faida ya shilingi 3,287,107,061 kwa watumiaji wa huduma yetu ya Airtel Money pamoja na mawakala nchi nzima. Hii ni mara ya pili kwa kampuni yetu kutoa gawio kwa wateja watu, ambapo mwaka jana tulitoa kiasi cha jumla ya shilingi Bilion 5.3”.
Tunaamini gawiwo hili la faida litawasaidia mamilioni ya wateja wetu kufanya mambo mbalimbali kulingana na mahitaji yao na hivyo kudhihirisha dhamira yetu yakutoa huduma bora za kifedha nchini. Tunaahidi kuendelea kuwawezesha wateja wetu kupitia huduma na bidhaa zetu kwa kuendelea kutoa huduma bora na za gharama nafuu za Airtel Money katika maeneo mbalimbali nchini”. Aliongeza Naligingwa
Huduma ya Airtel Money inawawezesha wateja kulipia ankra za huduma na bidhaa, kununua muda wa maongezi , kununua vifurushi vya data, kutuma na kupokea pesa , kutoa pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money , kutoa na kutoma pesa kutoka kwenye akaunti zao za benki na nyingine nyingi.
Airtel Money kupitia huduma ya Airtel Timiza imeendelea kuwa huduma ya kibunifu na yakuigwa kwa kutoa mikopo ya haraka , isiyo na dhamana kwa wateja na mawakala wa Airtel Money nchini. Huduma ya Airtel Timiza ni salama, haraka, rahisi kutumia , inapatikana siku 7 za wiki masaa 24 kupitia simu ya mkononi.
No comments:
Post a Comment