HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 28, 2016

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA:MTU MMOJA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

“PRESS RELEASE” TAREHE 28.01.2016.
· MTU MMOJA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI.

· MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI MKOANI MBEYA.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA CHILANGA WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA AITWAYE EMANUEL NZUNDA [55] ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI NA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU AITWAYE MENGO MKISI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.01.2016 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHILANGA, KATA YA IHANDA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. 

CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI, BAADA YA MAREHEMU KUMTUHUMU MTUHUMIWA KUWA NA MAHUSIANO NA MKE WAKE AITWAYE TELEZIA AZIMIO [31] MKAZI WA CHILANGA, AMBAYE AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO. 

INADAIWA KUWA, MAREHEMU BWANA EMANUEL NZUNDA [55] ALIPORUDI NYUMBANI TOKA KAZINI HAKUMKUTA MKE WAKE NA HIVYO KUAMUA KWENDA NYUMBANI KWA MTUHUMIWA NA KUMKUTA MKE WAKE AKIWA NA MTUHUMIWA NA NDIPO UGOMVI UKATOKEA. MAREHEMU ALIFARIKI KUTOKANA NA KIPIGO NA KUTOKWA NA DAMU NYINGI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI KWA UCHUGUZI ZAIDI WA KITABIBU. MTUHUMIWA ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MWENDESHA PIKIPIKI MKAZI WA MBIMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NELSON MSHEMWA [54] ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 998 DDL AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA KENEDY MJELWA [35] MKAZI WA MLOWO.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.01.2016 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KIJIJI CHA MBIMBA, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. 

CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 998 DDL AINA YA MITSUBISHI FUSO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. DEREVA WA GARI ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA NA KUHESHIMU SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA WA GARI AZITOE ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad