
Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Viongozi, wanachama
na wapenzi wa CHADEMA wa Tawi la Washington DC, Marekani, kutuma salamu za pole kwa familia ya
aliyekuwa Mbunge wa viti maalum Chadema Kupitia Jimbo la Kwimba Mheshimiwa
Leticia Nyerere (pichani) kilichotokea baada ya kuugua kwa muda mfupi hapa Maryland,
Marekani, siku ya Jumapili Tarehe 10
Januari 2016.
Kwa hakika tumepokea taarifa ya msiba wa mheshimiwa Leticia
Nyerere kwa mshtuko mkubwa kutokana na kumbukumbu ya mchango mkubwa aliyotoa
kwenye kufungua Tawi letu la Chadema hapa Washington DC, Marekani. Pia kwa
mchango wake aliyotoa akiwa kama mbunge wa Viti Maalum kupitia Chadema. Kwa
kweli bado tulikuwa tunahitaji sana mchango wake lakini mpango wa mungu hauna
makosa.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Leticia Nyerere
mahali pema
peponi, Amin.
Mwenyekiti wa CHADEMA Washington DC, Marekani
Kalley Pandukizi
No comments:
Post a Comment