Ni siku kadhaa zimepita toka lilipotimizwa agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kuadhimisha siku ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali yanayotuzunguka. lakini cha ajabu ni baada ya kumalizika kwa zoezi lile, hakuna tena kilichoendelea baada ya watu wengine kufanya usafi maeneo yao na kwenda kulundika uchafu huo kwenye maeneo ya watu na kuuacha hapo kana kwamba ndio sehemu iliyostahili kuuhifadhi uchafu huo. hi ni kweli kwamba na hili nalo ni mpaka Rais aseme kwamba baada ya kufanya usafi mkatupe uchafu kwenye maeneo husika?? hii ni sehemu moja tu kati ya nyingi nilizopita na kukutana na hali hii, kesho ntawaletea mtiririko wa matukio ya hivi katika maeneo mengine.
Sunday, December 13, 2015

Home
Unlabelled
ZOEZI LA USAFI LILIFANYIKA VYEMA NA MWISHO WAKE UKAWA HIVI
ZOEZI LA USAFI LILIFANYIKA VYEMA NA MWISHO WAKE UKAWA HIVI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment