HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 30, 2015

WAZIRI MKUU, MAJALIWA ATAKA MAELEZO JUU YA UBADHILIFU WA MALI ZA UMMA HALMASHAURI YA KIGOMA UJIJI

Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, Mhandisi na Mhasibu kupeleka taarifa ya maandishi kwa katibu tawala wa mkoa juu ubadhirifu waliofanya wa mali za umma.

Hayo ameyasema leo wakati akiongea na watumishi wa Wilaya zote kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF .

Alisema kuwa katika halmashauri ya Kigoma Ujijikuna ubadhirifu wa malu za umma umefanyika wa kuuza soki la Kigodeko,jengo la baby come na jengo la mi boss kwa kiasi cha shilingi milioni mia tatu badala ya milioni 800.

Alisema kuwa anawataka wajieleze kwa katibu tawala wa Mkoa kea maandishi ni utaratibu upi wametumia kuuza mali za umma na kwanini walikiuka agizo la mkuu wa Mkoa la kuwataka wasiuze mali hizo.

Majaliwa alisema kuwa maelezo yao anayataka jumamosi ya tarehe mbili yaweyamekamilika na kufika ofisini kwakwe ili kama kuna ukweli hatua za kinidhamu ziwe kuchukuliwa kwa waliohudika na ubadhilifu huo.

Akiongea na mtandao huu juu ya tubuma hizo mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji mhandisi Boniface Nyembele alisema kuwa ni kweli mali hizo wameuza lakini kwa kufuata utaratibu.

"Utaratibu wote tulifuata kuuza malu hizo na vikao halalu vilikaa na kupitisha na mihutasari ya vikao ipi na tenda tulitangaza tika mwaka 2013 tumeuza mwaka huu mwezi wa 6"alisema Mkurugenzi

Alisema fedha walizouza zilitumika katika ujenzi wa mahabara na shughuli zingine.

'Kwakuwa waziri mkuu ametutaka tujieleze kwa maandishikwa katibu tawala turafanya hivo kwani kila kitu kipo wazi"alisema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na watumishi kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Kigoma juu ya ziara yake ya kikazi Mkoani hapa.
Baadhi ya watumishi na viongozi wa mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa katika Kikao cha Majumuisho ya ziara yake mkoani humo kwenye ukumbi wa NSSF Desemba 30, 2015.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad