Wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za barani Afrika na Ulaya wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani. Warsha hiyo imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.
Dokta
Mwele Malecela wa Kituo cha Utafiti wa Madawa (NIMR) Tanzania akifanya
mahojiano jana na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoshiriki katika
warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za
kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama ukiwemo ugonjwa
wa Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko
duniani.Warsha hiyoimeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS
na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini
Ufaransa.
No comments:
Post a Comment