WATU kadhaa wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya Kampuni ya NEW FORCE ONE lenye namba za usajili T483 CTF kupinduka mapema mchana wa leo katika eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Morogoro, jitihada za kusafirisha majeruhi zinaendelea. Chanzo cha ajali hiyo, inaelezwa kuwa ni Lori la mizigo lililokuwa likitokea upande wa Morogoro, kupasuka tairi ya mbele na kupoteza muelekeo uliopelekea kuligonga basi hiyo na kupinduka. Glogu ya Jamii inafanya jitihada za kumpaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa kwa taarifa zaidi. tutaendelea kuwaletea taarifa kadri tutakavyozipata.
Sehemu ya Basi hiyo baada ya kupata ajali.
Inna lillah wa inna ilaih laajiun
ReplyDelete