HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 10, 2015

MTOTO HUYU ANATAFUTWA NA WAZAZI WAKE

MWANAFUNZI Evelina Edwin Kazaura (13), (pichani) wa shule ya msingi Dodoma mlimani, Manispaa ya Dodoma amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Kwa mujibu wa mzazi wa mwanafunzi huyo, Joyce Nchimbi, alisema mtoto huyo alitoweka nyumbani miezi mitatu iliyopita akiwa amevaa nguo hiyo.

Alisema mara ya mwisho alionekana mitaa ya Railways akiwa na wanafunzi wenzake lakini baada ya hapo hajaonekana tena.

Joyce alisema juhudi za kumtafuta mtoto huyo kwa ndugu na jamaa hazikufanikiwa na kutoa taarifa katika kituo cha polisi cha kati Dodoma na kufunguliwa jalada namba DOM/RB/5005/2015.

Joyce ameomba kwa yeyote atakayemuona mtoto huyo atoe taarifa kituo chochote cha  polisi au apige simu namba 0756- 365064 au 0654- 666755.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad