HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 26, 2015

Kampuni ya Ageco Energy & Construction Ltd yafunga mwaka kwa Kufunga Mtambo Mkubwa wa Sola Hospitali ya Mkoa Singida. Kampuni Ageco Energy & Construction Ltd ni kampuni ya kitanzania inayotoa huduma mbali mbali za ukandarasi ikiwemo ufungaji wa mitambo ya umeme wa jua (solar power) kwa watu binasfi, taasisi za umma, mashirika ya nje, na wateja wengine toka sekta binasfi.  Hivi majuzi Ageco ilikamilisha mradi wake wa mwisho wa mwaka kwa kufunga mtambo wa umeme wa sola ujulikanao kitaalamu kama solar hybrid backup system katika hospitali ya Mkoa wa Singida. 

 Mtambo huu wenye uwezo wa kuendesha vifaa vyenye jumla ya Kilowatt 15.7 utasaidia kutoa umeme kwa muda wa masaa 24 katika jingo la maabara la hospitali ya mkoa wa Singida hata kama umeme wa gridi ya taifa ukikatika. Mwezi wa Juni 2015, Ageco pia walifunga mtambo mwingine kama huu katika hospitali kuu ya mkoa wa Rukwa iliyoko Sumbawanga. Miradi hii imepewa ufadhili na Shirika la Misaada toka nchini Marekani linaloitwa Abbott Fund ambalo tayari limetoa misaada mingi katika kuimarisha sekta ya afya nchini Tanzania.

Ageco ni kampuni ya kitanzania inayotoa huduma za ufungaji wa mitambo ya umeme wa kawaida, umeme wa jua, umeme unaotokana na mabaki ya takataka (biomass) pamoja na huduma za ukandarasi wa majengo/nyumba na barabara.  Bei zao ni nafuu na wanatoa huduma kwa ustadi na weledi mkubwa. Wanapatikana kwa njia ya simu kupitia namba 0758 733 333 au 062 222 064. Vile vile wanapatikana kwa email kupitia info@agecoenergy.com. Ofisi zao ziko barabara ya Bima, Mikocheni B, jijini Dar es Salaam. Unaweza pia kutembelea tovuti yao www.agecoenergy.com kwa maelezo zaidi kuhusiana na huduma zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad