HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 10, 2015

DAWASCO YASAFISHA KARIAKOO

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO , Mhandisi Cyprian Luhemeja akishirikiana na wafanyakazi wa DAWASCO katika zoezi la usafi kwenye soko la Kariakoo katika maadhimisho ya siku ya Usafi kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Mecky Sadick pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiendelea na zoezi la usafi.

Shirika la majisafi na majitaka Dar es salaam(Dawasco) katika kutekeleza agizo la mh. Rais john pombe magufuli la kuadhimisha sherehe za uhuru kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali, leo DAWASCO imefanya usafi katika soko kuu la kariakoo lilipo wilaya ya ilala, jijini Dar Es Salaam, ikiwa ni jitihada za kupambana na ugonjwa wa kipindupindu ulioenea nchi nzima.

Usafi huo uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Mecky Sadick pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja ulifanya usafi katika maeneo yote muhimu ikiwemo sokon Shimoni, Mtaa wa Msimbazi na Uhuru pamoja na uzibuaji wa Mitaro ya Majitaka katika Mitaa ya Libya na Zanaki.

Akiongea katika usafi huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alisema usafi ni jukumu la kila mwananchi bila kujali itikadi yake na hivyo kuwahimiza wananchi kuwa na tabia ya kufanya usafi katika maeneo yao kuliko kusubiri kupewa maagizo na serkali.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO alisema siku hiyo wameiadhimisha kwa kufanya usafi katika soko la Kariakoo ambalo ni moja ya wateja wake ili kuwa mfano mzuri kwa wananchi na jamii nzima inayohudumiwa na Soko hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad