HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 12, 2015

DAR ES SALAAM, BAGAMOYO KUKOSA HUDUMA YA MAJI KESHO

Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linasikitika kuwatangazia  wakazi wa jiji la Dar-es-salaam na  Mji wa Bagamoyo kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa Saa 24 siku ya Jumapili, Tarehe 13/12/2015.

Mtambo wa Ruvu Chini utazimwa kutokana na matengenezo na Maboresho ya Njia kubwa ya Maji inayohudumia eneo la Salasala na viunga vyake vyote.

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo katika Jiji la Dar es salaam kukosa Maji:

MJI WA BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.
Maeneo Mengine ni : MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE) 

WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad