
Mrembo huyo ataondoka nchini Ijumaa ya tarehe 20 Novemba 2015 na ataungana na waremboe wengine kutoka nchi zaidi ya 120 duniani na watapiga kambi ya mwezi mmoja katika Hotel ya Beuaty Crown, Sanya nchini China.
Lilian amekuwa katika maandalizi ya kutosha tangu achukue Taji hilo mwezi Oktoba 2014.
Pamoja na mambo mengine ameshiriki Onyesho la Mavazi la nchi za Afrika ya Mashariki lililoandaliwa na Kampuni ya Arapapa Fashion ya mjini Kampala Uganda mwezi Novemba 2014 pia ameshiriki katika shughuli mbalimbali za Jamii katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Dar es salaam.
Kama Balozi wa Hospital ya CCBRT Miss Tanzania Lilian Kamazima ataondoka na ujumbe wa kupiga vita na kupambana na matatizo ya wasichana na akina mama ya Fistula.
Mrembo huyo anatarajia kurejea nchini tarehe 20 Desemba 2015.
No comments:
Post a Comment