.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Michael Mhondo akuzungumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) juu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wamesaini mkataba wa kutoa huduma za afya kwa wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari leo jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Michael Mhondo wakushoto na kulia ni Mkurugenzi wa PSPF Adam Maingu, wakisaini mkataba wa kutoa huduma za afya kwa wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari. leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Michael Mhondo na Mkurugenzi wa PSPF Adam Maingu,wakishikana mikono baada ya kusainiwa mkataba huo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Michael Mhondo na Mkurugenzi wa PSPF Adam Maingu, wakizidua huduma za afya kwa wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari. leo jijini Dar es Salaam.
MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma(PSPF) kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), wamesaini mkataba wa kutoa huduma za afya kwa wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa PSPF Adam Maingu alisema idadi kubwa ya wanachama wa uchangiaji wa hiari ni watanzania ambao wapo katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi kama waendesha bodaboda, mamalishe, wakulima, wafugaji, wasanii, wanamichezo na wajasiriamali.
Amesema baada ya kufanya utafiti waligundua kuwa matatizo makubwa yanayowakabili ni upatikanaji wa huduma za afya hivyo wamekubaliana na mfuko wa bima ya afya kwamba mwanachama atakayelipia kiasi cha Sh 76,800 atatengenezewa kadi ya bima ya afya na atapata huduma za afya kwa kipindi cha mwaka mmoja chini ya udhamini wa PSPF.
“Walengwa wakuu katika fao hili la matibabu ya PSPF ni wanachama wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari na wategemezi wao watano kwa kila mwanachama.
“Mwanachama wa PSPF atakayejiunga na mpango huo atanufaika na mafao yote ya bima ya afya sawasawa na mwanachama mwingine yeyote wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
“Huu ni mpango wa aina yake katika sekta ya Hifadhi ya Jamii hapa nchini, kwani mnufaika atapatiwa kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kuweza kupatiwa huduma ya matibabu nchi nzima kwenye vituo vyote vilivyosajiliwa na NHIF kuanzia Hospitali ya Taifa, rufaa, Hospitali za binafsi, mikoa, vituo vya afya na zahanati zote za Serikali.
“Pia huduma hiyo itakuwepo katika vituo vya mashirika ya dini na binafsi pamoja na maduka ya dawa yaliyosajiliwa na PSPF,”alisema Maingu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Muhando, alisema kusainiwa kwa mkataba huo utawanufaisha wananchi wengi waliojiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali vikiwemo vya umoja wa madereva wa malori, wavuvi, wakulima pamoja na vyama vya waandishi wa habari.
“Lengo ni kuwajengea uwezo wajasiriamali kuwa na maisha bora, na vikundi 38 tayari tumeshavisajili na mfumo wa awamu ya tano wa ‘Hapa kazi tu’ tunautekeleza kwa kasi” alisema Muhando.
Almesema mfuko wa NHIF ulianzishwa kwa ajili ya kuwezesha watu kuchangia huduma za matibabu kabla ya kuugua na tangu tangu mfuko huu ulipoanza shughuli zake mwaka 2001 umekuwa ukipanua wigo wake kwa kusajili makundi ya aina mbalimbali ili kufikia lengo la Serikali afya bora kwa wote.
No comments:
Post a Comment