Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli
akikagua gwaride maalum la Jeshi la Ulinzi lenye Umbo la Alfa, ikiwa ni
ishara ya kuanza kwa Serikali mpya ya awamu ya tano, katika Sherehe za
kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
salaam leo. Sherehe hizo zimehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa ndani
na nje ya nchi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akila
kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh. Mohamed Chande Othman, katika
Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini
Dar es salaam leo.Kushoto ni Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Makamu wake, Mh. Dkt. Mohamed Gharib
Bilal. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Rais
aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davies Mwamunyange, wakati
akiwaaga wananchi mara tu alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa, katika
Sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe
Magufuli, zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.
Rais
aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu ya
heshima ya kijeshi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais Mpya wa awamu
ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt.
John Pombe Magufuli akionyesha Mkuki na Ngao aliokabidhiwa na Wazee wa
kimila ikiwa ni ishara ya Uongozi wa Kitaifa, katika Sherehe za
kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
salaam leo.
No comments:
Post a Comment