Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Sunrise ya mjini Mwanza Janeth Malima akionyesha kipaji cha kucheza kwenye tamasha la Coke Studio lililofanyika shuleni hapo.
Wanafunzi wa shule za sekondari za Bwiru na Sunrise wakionyesha vipaji vyao vya kucheza na kuimba wakati wa tamasha la Coke studio.
Wanafunzi wakifuatilia burudani za tamasha la Coke Studio wakiburudika na kinywaji cha Coca-Cola
- Mwanza,Dar,Mbeya na Arusha waonyesha vipaji vyao vya kuimba
Msimu wa Coke studio mwaka huu ambao unajumuisha kolabo ya wanamuziki wa Tanzania na wanamuziki kutoka nje ambao umezinduliwa mapema wiki iiyopita unazidi kuleta burudani katika makundi mbalimbali ya jamii ambao wanafunzi wa sekondari wamepata fursa ya kushiriki na kuonyesha vipaji vyao vya kucheza na kuimba.
Katika matamasha yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika mikoa ya Arusha,Mbeya,Mwanza na Dar es Salaam wanafunzi kutoka shule mbalimbali waliweza kushiriki burudani za matamasha ya Coke studio na kuonyesha vipaji vyao vya kuimba na kucheza.
No comments:
Post a Comment