Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano kongamano la kuchochea uzalishaji mali, Prof.Leonard Mwaikambo akizungumza na waandishi wa habari juu ya lengo la kongamano ni kutoa fursa kwa watanzania kwa jumla kuelewa malengo na mwelekeo wa taifa letu kufikia uchumi wa kati .
Na Emmanuel Massaka ,Globu ya Jamii
RAIS Dk. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kuchochea uzalishaji mali katika kuinua kipaato cha mtanzania wa kawaida kufikia malengo ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 litakalofanyika kesho katika Ukumbi Diamond Jubilei jijini Dar es Salaam.
Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano Prof.Leonard Mwaikambo kongamano hilo litakuwa na watoa maada mbalimbali na wataalam katika sekta ambazo zitafanya kufikia uchumi huo.
Profesa Mwaikambo amesema kuwa wakati huu kutokana na harakati za uchumi kunahitajika wataalam ambao wamebobea kwa kuleta maendeleo hayo ambayo watanzania wanayoyataka kwa kukuza kipato.
Amesema kongamano hilo linagusa nyanja zote katika sera za vyama hivyo ni muda mwafaka wa kujadili masuala ya uchumi ni ya msingi katika ukuza ji kipato kwa wananchi.
Aidha amesema wanataaluma hao watatoa mchango wao katika maswala ya kijamii na sekta mtambuka , Utawala Bora ,na Mawasiliano ya kielektroniki kwa ukuzaji wa maendeleo watanzania ,Miundombinu ,Afya ,Maji, Elimu pamoja na ujenzi .
Majadiliano yataongozwa na Waziri Mkuu Mstaaf,Jaji Mstaafu,Joseph Sinde Warioba na neno la shukrani litatolewa na Waziri Mkuu,Mstaafu, John Malecela .
No comments:
Post a Comment