Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya kuwakaribisha
nchini wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika
katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) kabla
ya kufungua kikao cha wajumbe hao kinachofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff,
Zanzibar. Lengo la kikao hicho ni kujadili
masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa
Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout,
Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini,
Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wajumbe
wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa
katika chumba cha mkutano wakijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano
ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo
ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda,
Sudan, Sudan ya Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Mkutano
huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar
ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) ndio Mwenyekiti
wa Baraza hilo, hata hivyo katika Mkutano huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia meza kuu) anamuwakilisha katika kikao hicho.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika
katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini, Pereira Ame Silima (kulia) akiwa
na Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Uganda
ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi James Baba (katikati) na
Mjumbe wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani
nchini Rwanda, Balozi Munyabagisha Valeus, wakisoma taarifa za masuala
mbalimbali ya jinsi ya Kupambana ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha
Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia,
Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika
ya Kati, Somalia na Tanzania. Baraza hilo limekutana katika Hoteli ya Sea
Cliff, Zanzibar leo. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika
katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi nchini, Pereira Ame Silima (katikati
waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo ambalo nchi
zake wanachama ni Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan,
Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Wajumbe
hao wamekutana katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:
Post a Comment