HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 22, 2015

KUTOKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR: YANGA YABEBA NGAO YA JAMII

 Kikosi cha Timu ya Yanga, kikishangilia kwa pamoja ushindi wao mara baada ya Ngao ya Jamii yenye kuashiria kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, katika mtanange uliopigwa jioni hii dhidi ya Timu ya Azam, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga imepata ushindi huo kwa mikwaju ya penati 8-7, baada ya dakika tisini za mchezo kumalizika bila kufungana.
Wachezaji wa Timu ya Yanga, wakishandilia ushindi wao huo pamoja na mashabiki wao wakuojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kushabikia timu yao iliyokuwa ikikipiga na Timu ya Azam. Yanga imepata ushindi huo kwa mikwaju ya penati 8-7, baada ya dakika tisini za mchezo kumalizika bila kufungana.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amis Tambwe akiondoka na mpira mara baada ya kumpiga chenga ya mwili Beki wa Timu ya Azam, Pascal Wawa (aliekaa chini) wakati wa mtangange wa kuwania Ngao ya Jamii ya Ufungunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hakuna timu iliyoona lango la mwenzie mpaka dakika hii.
Kiungo machachari wa Azam, Farid Mussa akiangalia namna ya kumtoka, Geofrey Mwashiuya wa Yanga, wakati wa mtangange wa kuwania Ngao ya Jamii ya Ufungunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hakuna timu iliyoona lango la mwenzie mpaka dakika hii.
Beki wa Azam, Pascal Wawa akionyesha umahiri wake wa kuondosha hatari langoni kwake mbele ya Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe.
Mchezaji wa Timu ya Yanga, Thaban Kamusoko akiruka kuwania mpira wa juu mbele ya Frank Domayo wa Azam, wakati wa mtangange wa kuwania Ngao ya Jamii ya Ufungunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hakuna timu iliyoona lango la mwenzie mpaka dakika hii.















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad