Madereva wa bajaji jijini Mbeya, Mapema wameandamana kuanzia eneo la Mafiati kuelekea Mwanjelwa huku wakichoma moto mataili ya gari kwenye baarabara kuu Tunduma katika makutano ya eneo hilo, kwa madai ya kwamba wanahitaji wapewe ruhusa ya kutembea na kuruhusiwa kupita barabara kuu na kupunguziwa mapato ya ushuru wa bajaji hizo, hali ya usalama ilitetereka kidogo mjini hapa, hadi pale jeshi la polisi lilipofika kutuliza gasia kwa kupiga mabomu ya machozi kukabili hali hiyo.picha zote na Fadhiri Atick globu ya jamii Mbeya.
Hapa heka heka ya baadhi ya madereva wa bodaboda na bajaji wakiwa wanachochea moto huku wakiimba na kushangilia jambo hilo.
baadhi ya matairi yaliyo tiwa kibiriti yakiendelea kuwaka kandokando ya barabara.
baadhi ya madereva wa bajaji wakiendeleza mgomo wao.
"hii ni mtaa kwa mtaa mpaka kieleweke."
"tunacho taka ni kuruhusiwa tuu kupiga kazi barabara kuu vinginevyo tunaendelea kukinukisha..."
hapo baadhi ya viongozi wa bajaji wakidhadhiana na jeshi la pilisi.
polisi wakiendelea na uturizaji gasia eneo la mafiati mbeya.
Hali ni tete hiii.......
baadhi ya madereva wa bodaboda wakishuhudia tukio hilo.











No comments:
Post a Comment