Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkomo maelfu ya wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Mpanda, waliofurika kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi leo Juni 14, 2015.Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu zenye majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Katavi leo Juni 14, 2015, waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Bi. Elizabert Kashira. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah akizungumza machache mara baada ya Mh. Lowassa (pili kulia) kukabidhiwa fomu za wadhamini wa CCM za kumuwezesha kutata ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Wengine pichani toka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Dkt. Aman Kaburou pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda, Beda Katani.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na wanaCCM wa Mji wa Sumbawanga, Mkoani Rukwa wakati alipofika kutafuta udhamini wa kupewa ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya wanCCM 4045 wamemdhamini.
No comments:
Post a Comment