HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 1, 2015

MWANAHABARI MKONGWE AFARIKI DUNIA

Mwandishi mkongwe wa habari, Kyaloeichi Oko Kessy (62) amefariki dunia usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Pugu jijini Dar es Salaam.

Mpwa wa marehemu Tumaini Msengi amesema hayo leo kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu kwa muda mrefu na amekuwa akitibiwa katika hospitali mbalimbali za jijini Dar es Salaam hadi jana ambapo mauti yalimkuta.

Kabla hajaanza kuugua Kessy alikuwa mwandishi wa kujitegemea akiandika zaidi uchambuzi na makala katika vyombo mbalimbali vya habari nchini yakiwemo magazeti ya Motomoto,Shaba,Rai, na mengineyo mengi pia alikuwa ni mtunzi wa vitabu vya aina mbalimbali.

Msengi ameeleza kuwa marehemu ameacha watoto wawili na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mdogo wake Chanika nje kidogo ya jiji na mazishi yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Marehemu ni mzaliwa wa kijiji cha Rosho Kilema mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad