Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na vijana ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwapokea vijana hao walipofika kijijini Kilemba ili wapelekwe kambini baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga tarehe 17 Mei, 2015.
Baadhi ya vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwa wamepunzika kijiini Kilemba kabla ya kusafirishwa na basi kwenda kwenye kambini mara baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga tarehe 17 Mei, 2015.
Mkuu
wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya (mwenye koti) akipata
maelezo ya njia ya kutembea kwa miguu kutoka Kagunga hadi Mkigo kutoka
kwa mkazi wa kijiji hicho, Mahmud Ahmad wakati alipokagua njia hiyo ili
itumike kuwasafirisha waomba hifadhi ya ukimbizi wa Burundi, tarehe 17
Mei, 2015, (mwenye Kaunda suti ) ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa
Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya.
Mkuu
wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya (mwenye koti) akiwa
katika kijiji cha Kilemba kwa ajili ya kuwapokea waomba hifadhi ya
ukimbizi wa Burundi waliokuwa wanasafirishwa kwa kutembea kwa miguu
kutoka kijiji cha kagunga hadi kijijini hapo ili wapelekwe kambini
(mwenye Kaunda suti ) ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya
Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya, Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi
24 KJ Kigoma, Luteni Kanali Donald Msengi (katikati) na Kaimu Katibu
tawala wa mkoa wa Kigoma, Salvatory Shauri tarehe 17 Mei, 2015.
Mkurugenzi Idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen, Mbazi Msuya akiongea na mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la kusafirisha wakimbizi, Son Ha Dinh, mara baada ya kuwasafirisha vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi kutoka kijiji cha kagunga, tarehe 17 Mei, 2015.

No comments:
Post a Comment