HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 1, 2015

HIVI USHAWAHI KUJIULIZA NI NINI CHANZO CHA HIZI FOLENI ZA JIJI LA DAR??

Ukiangalia kwa makini picha hii utabaini kuwa kuna uzembe mkubwa sana unafanywa na baadhi ya madereva, ambao kwao haraka ndio kitu kinachopewa kipaumbele kuliko kufuata taratibu za utumiaji wa barabara, yaani hawana ustaarabu kabisa na hawapendi kufuata sheria. kwa mfano hapa kulikuwa kuna ulazima gani wa kuleta foleni yote hii?? Pamoja na kwamba kuna mafanu wanaendelea na shughuli zao lakini haikuzuia magari kupita, kwani wangekuwa wanasubriana na kupeana nafasi pia kutumia njia moja kama inavyotakiwa katika barabara hizi, sidhani kama kungekuwa na nyororo refu namna hii linalopeleke kukaa barabarani zaidi ya masaa matatu mpaka manne ndio mtu afike anakokwenda.
 Haya hapa zimeanzishwa njia mbili zisizokuwa na ulazima wowote, maana wanaoteka upande mwingine hawana nafasi tena hapo.
Haya huyu nae sijui katokea wapi, kawaletea jeuri wennzie na kupelekea foleni kuwa kubwa, ila alipomuona Trafiki sasa analazimisha kuingia njia kuu baada ya kuona mchepuko ushaingia ruba.
 Haya hapa tena yale yaleee....

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad