
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongizi wengine wakiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia) baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Baba Askofu wa Anglikan wa Kanisa la Mkunazini Michael Hafidh akiomba dua wakati Viongozi mbali mbali waliofika katika kaburi la aliyekua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai maara
alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
kubhudhuria katika Hitma ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee
Abeid Amani Karume Iliyofanyika leo asubuhi.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa
Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua
iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini
Zanzibar leo asubuhi.
Makamo
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilali
akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa
Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua
iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini
Zanzibar leo asubuhi.
Muasisi
wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir akiweka shada la mauwa katika
kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani
Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa
Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Balozi
Ali Karume (Mtototo) kwa niaba ya familia akiweka shada la mauwa katika
kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani
Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa
Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Wake
wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa katika kaburi la Marehemu
MzeeAbeid Amani Karume baada ya hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa
Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja na kuhudhuriwa na waislamu mbali
mbali Mjni na Vijijini.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein(katikati) akiwaongoza Viongozi mbali mbali pamoja na Wananchi
katika Kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu
Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.
Baadhi
ya Viongozo wakisoma hitma akiwemo aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar
Marehemu Mzee Abeid Amani Karume(kushoto) Balozi Ali Karume katika
ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo
asubuhi.
Waislamu
na wananchi mbali mbali wakiwa katika kisomo cha hitma ya aliyekuwa
Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika
ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo
asubuhi.
Akinamama
wa Mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja wakiwa katika kisomo cha Hitma ya
aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika
leo asubuhi.
Mke
wa Rais Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na Mama Shadya
Karume Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar(wa tatu kulia) Mama Fatma Karume
(wa pili kulia) Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Zakia
Bilali (kushoto) Bi Khadija Aboud (wa pili kushoto)Mjumbe wa Kamati Kuu
wa CCM,katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu
Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM
Kisiwandui Mjini Unguja.(Picha na Ikulu, Zanzibar.)













No comments:
Post a Comment