HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 2, 2015

HAFLA YA KIKUNDI CHA WAHITIMU WA CHUO CHA MZUMBE WALIOMALIZA MASOMO KATIKA KIPINDI KATI YA MWAKA 1992 NA MWAKA 1996 YAFANA

1Kaimu Mkuu wa Chuo Mzumbe Prof. Josephat Itika akizungumza katika hafla ya kikundi cha wahitimu wa chuo cha Mzumbe waliomaliza masomo katika kipindi kati ya mwaka 1992 na mwaka 1996 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
2Wahitimu wa chuo cha Mzumbe waliomaliza masomo katika kipindi kati ya mwaka 1992 na mwaka 1996 wakimsikiliza Prof. Josephat Itika wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
3 4Wana kamati waliondaliwa kwaajili ya kufungua shampeni wakati wa hafla hiyo.
5Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Mzumbe Prof.Faustin Kamuzora (kushoto), akisalimiana na Gerald Mwanilwa ambaye ni Mwenyekiti wa chuo hicho (katikati) Mwenekiti wa wahitimu hao Bw. Emmanuel Ngallah, na wakwanza kulia Mweka Hazina wa kikundi hicho Bi. Jane Mwakalebela.
6Bi. Jane Mwakalebela, akiwa na mumewe Mwakalebela wakiwa katika picha ya pamoja.
7wahitimu wa chuo cha Mzumbe waliomaliza masomo katika kipindi kati ya mwaka 1992 na mwaka 1996 wakigonga cheeasi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

8Kaimu Mkuu wa Chuo Mzumbe Prof. Josephat Itika (kulia), wakifurahia jambo na wahitimu wa chuo cha Mzumbe.
9
picha ya pamoja.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON.
............................................................................... 
IDADI ya wanafunzi wanaosma katika chuo kikuu cha Mzumbe imeongeza kutoka kati ya 900 na 1000 mwaka 1994 hadi kufikia 12,280 hivi sasa. Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Josephat Itika amesema ongezeko kubwa la wanafunzi imetokana na sifa nzuri ya chuo na juhudi kubwa za uongozi wa chuo.

Akizungumza katika hafla ya kikundi cha wahitimu wa chuo hicho waliomaliza masomo katika kipindi kati ya mwaka 1992 na mwaka 1996 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Prof. Itika amesema kuwa kampasi kuu ya Chuo iliyopo mjini Morogoro ina wanafunzi zaidi ya 7,500.

"Tumefanya kazi kubwa tangu mlipohitimu, kwa mfano, tunazalisha wahitimu wa shahada ya kwanza wasiopungua 4,000 kila mwaka. Tunazalisha wahitimu wasiopungua 2,800 wa shahada ya uzamili kila mwaka, hii ni hatua kubwa" alieleza Kaimu Mkuu wa Chuo huyo.

Prof. Itika alisema kuwa, kwa sasa chuo kina programu 23 na kila mwaka kinaanzisha programu mbili, lengo likiwa kukifanya kuwa bora. "Chuo cha Mzumbe ni mama wa menejimenti nchini, hii haina ubishi na mnapaswa mjivune kuwa zao la chuo hiki.

Nchi zilizoendelea, huwezi kuwa somebody (fulani) kama hutoki kwenye mtandao wa wahitimu mahiri. Mfano vyuo maarufu kama Exford, Harvard na Cambridge vinaimarisha mtandao wa wahitimu wake ili viendelee kubaki bora" alifafanua.

Prof. Itika alisema kuwa kutokana na umuhimu wa mtandao huo, Chuo Kikuu cha Mzumbe kimeamua kuwa na siku maalum ya wahitimu wake.

"Tayari tumeunda sekretarieti kwa ajili ya shughuli hiyo na huenda hafa hiyo ikawa kati ya mwezi Agosti au Septemba mwaka huu. Itakuwa siku nzuri, fikiria unakuja chuo na kulala chumba ulichokuwa unalala miaka 20 iliyopita" alieleza.

Kwa mujibu wa Prof. Itika, watu mbalimbali maarufu kama Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Ombeni Sefue, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo na aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu Bw. Ludovick Utouh wameonyesha nia ya kushiriki hafla hiyo.

  Kwa upande wake, Mwenekiti wa wahitimu hao Bw. Emmanuel Ngallah alisema lengo la kuanzishwa umoja huo lilikuwa ni kukutana na kubadilisha mawazo na taarifa, na baadaye kuwa na malengo makubwa zaidi.

"Tumeanza na hili la kukutana na kuweza kuwasiliana, tutatengeneza sera na mipango ili tuweze kufanya mabo makubwa zaidi kwa ajii yetu, chuo na Taifa kwa ujumla.

Kila mmoja wetu hapa ana nafasi, kipaji na rasilimali fulani ambavyo tukiviunganisha tutafanya kitu kikubwa" alifafanua.

Naye Mweka Hazina wa kikundi hicho Bi. Jane Mwakalebela amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa sana kwani hata wahitimu waliopo nje ya nchi wameonesha nia ya kujiunga na kikundi hicho.

"Kuna wahitimu wenzetu waliopo nje ya nchi wameomba tuandae mkutano mwingine ambao utawawezesha kushiriki na baadhi yao wametoa hadi michango kwa ajili ya kikundi hiki" aliongeza Ms. Mwakalebela.

Baadhi ya watu maarufu ambao ni zao la chuo cha Mzumbe ni pamoja na Balozi Sefue na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Anne Makinda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad