HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 17, 2015

SITTI MTEMVU ATEMBELEA KITUO CHA WENYE ULEMAVU WA NGOZI DAR ES SALAAM NA KUTEMBELEA HOSPITALI YA MKOA ILALA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The Sun Tanzania,Vicky Ntetema (kulia) akifafanua jambo wakati akizungumza na Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu (kushoto) alietembelea katika ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam,ili kuona namna ya Mfuko huo utakavyoweza kufanya kazi kwa pamoja na Shirika hilo katika kupiga vita mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.
Afisa utetezi wa Shirika la Under The Sun Tanzania,Kondo Seif (kushoto) akitolea malezo ya ukosefu wa rangi asili mwilini ambayo huathiri rangi ya mwili kwa maana ya ngozi ,macho na nywele na kukosekana kwa melani mwilini, miongoni mwa athari zake ni wepesi wa kuungua na Jua unapotembea na ufanyapo kazi juani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The Sun Tanzania,Vicky Ntetema (kulia) akimuonyesha Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu (kushoto) Picha ya mtoto alie tekwa akiwa mgongoni mwa mama yake ambaye aliathiriwa vibaya sana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The Sun Tanzania Vicky Ntetema (kulia) akionyesha picha ya Wazazi walio zaa watoto mwenye albinizim ambao kwa pamoja wameamua kuwalinda na kuwalea kwa pamoja.
Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The Sun Tanzania,Vicky Ntetema (kulia) Kofia na kitita cha Sh. Laki 3 kama mchango wake katika kusaidia kuendelea na kazi ya kuwalinda watu wenye albinizim.
picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu (wa tatu kulia) akimkabidhi vifaa vya kuhifadhia taka pamoja na sabuni,Mbunge wa Jimbo la Ilala,Mussa zungu ( wa pili kushoto), kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Ilala Dar es Salam.Wengine pichani kuanzia kushoto ni Diwani wa kata ya Kinyerezi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Leah Mgitu,Mama mzazi wa Sitti,Bi. Mariam Mtemvu, Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Mkoa Ilala,pamoja na Diwani wa Kata ya Ilala kupitia Chama cha Mapinduzi,Edson Fungo.
Mbunge wa Jimbo la Ilala,Mussa Zungu akiongea na Waandishi wa Habari ( hawapo pichani) mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya kuhifadhia taka na Sabuni kutoka kwa Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu.
Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu alipo tembelea wagonjwa Hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad