Afisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), Bw. Ntandu Mathayo (mwenye shati jeupe), akiwaonyesha wawekezaji kutoka nchini Marekani, gati namba 1 mpaka 7 inapoanzia katika bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi wakati wawekezaji hao walipotembelea bandari ya Dar es Salaam kuangaliza fursa za uwekezaji katika bandari ziizoko.
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Miundombinu wa Mamlaka ya Usimamizi wa BAndari
Tanzania, Mhandisi Alois MAtei, akiwaonyesha wawekezaji kutoka nchini
Marekani, eneo la Bandari ya Dar es Salaam, leo asubuhi walipotembelea
Bandari ya Dar es Salaam kuona fursa za kuwekeza katika sekta ya
Uchukuzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya kufua umeme ya TANASI, William Crawford (mwenye
tai ya blue), akimtambulisha mjukuu kwake Colin Machamsoc kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, mara baada ya
kuwasilia Wizarani hapo walipotembelea Leo Asubuhi kutaka kufahamu fursa
zilizo za uwekezaji katika Wizara ya Uchukuzi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, akisisitiza jambo kwa kundi la wawekezaji
kutoka nchini Marekani waliotembelea Wizara hiyo leo asubuhi, kutaka
kufahamu fursa za uwekezaji katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Uchukuzi, wawekezaji hao wameonyesha nia ya kuwekeza katika miradi ya
Viwanja vya Ndege, Bandari pamoja na reli.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathimini wa Wizara ya
Uchukuzi, Bw. Aunyisa Meena, akiwasilisha mada kwenye mkutano wa
uliowakutanisha wawezekezaji kutoka nchini Marekani waliotembelea Wizara
ya Uchukuzi leo asubuhi kutaka kufahamu fursa za uwekezaji zilizo
katika sekta ya Uchukuzi.
Robert
Shumake kutoka Kampuni ya Shukame Rails akikabidhi mchoro wa Treni za
mwendo kasi Diesel Multiple Unit (DMU) ambazo inataka kuwekeza katika
sekta ya Reli kwa Dkt. Shaaban Mwinjaka, wakati alipomtembelea Wizarani
kwa ajiili ya kuangalia fursa za kuwekeza katika sekta ya Uchukuzi.
Kampuni hiyo iko kwenye hatua za mwisho za kusaini Memorandum of
Understanding (MoU) na Shirika la Reli Tanzania (TRL), kwa ajili ya
kutengeneza treni hizo zitakazosafirisha abiria kati ya 800 mpaka 1000.(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
No comments:
Post a Comment