Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzunduzi wa Mbio za Uhuru Marathon,uliofanyika leo kwenye hoteli ya Kebby's,Mwenge jijini Dar es Salaam.Mbio hizo ambazo zinaenda sambamba na Maadhimisho ya Uhuru wa Taifa letu la Tanzania,zitafanyika Desemba 7,2014 katika viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es salaam.Kulia ni Mratibu wa Mbio za Uhuru Marathon,Innocent Melleck.
Mratibu wa Mbio za Uhuru Marathon,Innocent Melleck akizungumzia maandalizi ya mbio hizo na namna ya washiriki waakavyoweza kujiandikisha,ambapo amesema kwa wale wanariadha ambao wako nje ya nchi wanaweza kujiandikisha kupitia tovuti rasmi wa mbio hizo,ambayo ni www.uhurumarathoni.com.Wengine pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania,Bi. Ombeni Zavala.
Baadhi ya wanahabari wakifatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa.Picha na Othman Michuzi
Na Daudi Manongi
Chama cha Riadha Tanzania kimetakiwa kuwajengea wachezaji fikra chanya na maandalizi bora ili waweze kupata mafanikio katika mashindano ya Kimataifa na Kitaifa.
Hayo yamebainishwa leo na Naibu katibu mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokuwa akifungua Mbio za Riadha za Uhuru zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni jijini Dar es Salaam.ambazo zitafikia kilele chake 7/12/2014 katika viwanja vya leaders mjini dar es salaam.
Alisema michezo ya Riadha itumike kama daraja katika jamii kwa ujumla ili iweze kujenga mahusiano mema, kudumisha amani na kuenzi Muungano wetu.
Alitoa rai kwa viongozi wa riadha Tanzania kusimamia vyema mchezo huo ikiwa ni pamoja na kutafuta vijana wenye vijana ili kuweza kupata vijana bora ambao watashiriki karika mashindano mbalimbali ya ngazi tofauti yatakayofanyika nchini na nje ya nchi.
Wakati huohuo amewaasa wadau,wafadhali na taasisi mbali mbali kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza na kuchangia michezo mbalimbali ikiwemo kusaidia mafunzo na vifaa wakati wa mashindano.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Zainab Mbilo alisema michezo ni nguzo kuu katika kupunguza magonjwa na kuweka mwili katika hali nzuri pamoja na kusisitiza kwamba michezo inaleta umoja kwani hukutanisha watu wa rika tofauti katika jamii.
Nae mratibu wa mashindano hayo Bw. Innocent Melleck aliishukuru serikali kwa kuwapa moyo,mwongozo katika maandalizi ya mbio hizo kila yanapofanyika na kuyafanya kuwa bora
“Riadha ni mchezo ambao umewahi kuiletea nchi medali nyingi kwenye michezo mbalimbali ya kimataifa, ikiwamo Michezo ya Jumuiya ya Madola, Olimpiki na ya Afrika”. Alisema Bw. Melleck
Uhuru marathon ni tukio ambalo huadhimisha Siku ya Uhuru wa Tanzania huku ikiweka mkazo katika kuimarisha Amani,Upendo na Umoja.
Mwaka huu zitajumuisha mbio ndefu za kilometa 42,mbio fupi za kilometa 21 pamoja na kilometa 3 zitakazojumuisha viongozi ili kuonyesha uzalendo zikiwa mbio za tatu kufanyika tokea kuanzishwa kwake.
No comments:
Post a Comment