Group la Kandanda
katika Mtandao wa Facebook tarehe
25/10/2014 litakuwa likitimiza miaka 4 tangu kuanzishwa ndani ya facebook.
Kuadhmisha siku hiyo, Members
wa Kundi hilo wametengeneza timu ambazo ni #TeamDizomoja na #TeamIsmail, ambazo
zitachuana siku hiyo katika viwanja vya TCC Sigara-Chang’ombe.
Timu hizo zote mbili zimekuwa na maandalizi ya Takribani
Miezi miwili sasa, na usajili ulishafungwa tarehe 11/10/2014.
Sherehe hizo zinatarajiwa kuanza saa 3 Asubuhi ikifuatiwa na
Offline Socializition ya members wa kundi hilo ambao hutumia 24/7
kujadili masuala ya soka katika Facebook.
Kamati ya maandalizi inawakaribisha wanakandanda wote kwa
makabila (Timu) tofauti popote mlipo katika viwanja hivyo vya TCC Sigara,
usisahau Jezi yako tuu! Ndicho kitambulisho cha Kabila zetu (timu zetu).
No comments:
Post a Comment