
Mkuu
wa kitengo cha Sayansi ya Makosa ya Jinai Kemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa
Serikali Bw. Elias Mulima akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu
matumizi ya dawa aina ya Cocaine hospitalini kama tiba hasa kwa wagonjwa wenye
maumivu makali na wanaofanyiwa upasuaji, wakati wa Mkutano uliofanyika Leo
Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Makosa ya
Jinai na Vinasaba kutoka Ofisi hiyo Bi.Gloria Omari.(Picha
na Hassan Silayo -MAELEZO)
Na
Fatma Salum MAELEZO
Wakala
wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kubaini jumla ya kilogram
6,428.12 za sampuli mbalimbali za dawa za kulevya kwa kipindi cha kuanzia
Januari hadi Desemba 2013.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Makosa ya Jinai na Vinasaba
kutoka Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bi.Gloria Omari katika
mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Bi
Gloria alisema kuwa kiasi hicho cha madawa kimepatikana baada ya uchunguzi wa
majalada 208 yaliyopokelewa na kufanyiwa uchunguzi katika mwaka huo.
“Wakala
wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali umefanya Uchunguzi wa vielelezo
vidhaniwavyo kuwa ni dawa za kulevya ambapo majalada 208 yaliyopokelewa kwa mwaka
2013 na kubaini jumla ya kilogram 6,428.12 za dawa hizo”Alsema Bi. Gloria.
Akitaja
idadi ya majalada na sampuli za dawa hizo Bi Gloria alisema kuwa dawa aina ya
Bangi imeongoza kwa kuwa na kiasi kikubwa cha uzito wa sampuli ikiwa na
kilogram 3765.12 kwa idadi ya majalada 72 wakati Heroin imeongoza kwa kuwa na
idadi kubwa ya majalada ambapo majalada 112 yalichunguzwa na kilogram 46.67
ziligunduliwa.
Aina
nyingine ya dawa zilizotajwa ni Cocaine ikiwa na idadi ya majalada mawili
yaliyochunguzwa na kilogram 4.22 ziligunduliwa, majalada 21 ya mirungi yalichunguzwa
na kupatikana kilogram 2579.8 na jalada moja la Ephedrine lilikuwa na kilogram
32.31.
Bi
Gloria aliongeza kuwa shughuli za uchunguzi wa sampuli za dawa hizo umesaidia
utoaji wa ushahidi mahakamani pamoja na kupambana na usafirishaji wa dawa za
kulevya.
Akijibu
swali la waandishi wa habari Mkuu wa
kitengo cha Sayansi ya Makosa ya Jinai Kemia kutoka Ofisi hiyo Bw. Elias Mulima alibainisha kuwa kuna uhalali wa matumizi ya dawa aina ya
Cocaine hospitalini kama tiba hasa kwa wagonjwa wenye maumivu makali na
wanaofanyiwa upasuaji.
No comments:
Post a Comment