Meneja wa Kanda ya Kinondoni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahara Kayugwa akitoa mada wakati wa semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Penhsheni wa PPF kwaa Waajiri wa Makampuni na mashirika mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Seaescape, Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam leo.
Majaliwa E Mkinga, Mchambuzi na Mtengenezaji wa Mifumo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akielezea jinsi PPF ilivyotengeneza mfumo wa kupata taarifa za wanachama kupitia simu aina za Smartphone na kuutaja mfumo huo kuwa ni PPF TAARIFA App ambayo mteja ataweza kuiweka katika simu yake ya mkononi.
Baadhi ya waajiri wakielekeza kuhusu jinsi ya kuweka mfumo wa PPF Taarifa katika simu zao za Smartphone leo katika semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Seascape hotel Mbezi beach Jijini Dar Es Salaam.
Baadhi
ya Waajiri kutoka Mashirika na makampuni mbalimbali wakifuatilia kwa
makini mada zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wafanayakazi wa Mfuko Wa
Pensheni wa PPF.
Meneja wa Kanda ya Kinondoni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahara Kayugwa akiwaelezea waajiri waliohudhuria semina iliyoandiliwa na mfuko wa pensheni wa PPF leo jinsi kanuni mpya inavyofanya kazi kwa wanachama ili kuweza kupata mafao yao kutoka mfuko wa pensheni wa PPF.
Prof.
Betria Mapunda ambae amemwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es
salaam akifungua semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa
Waajiri kwa lengo la Kutoa elimu juu ya huduma zitolewazo na mfuko huo
wa Pensheni wa PPF katika ukumbi wa Seaescape, Uliopo Mbezi Beach Jijini
Dar Es Salaam.
Mmoja wa waajiri akiuliza swali kwa Meneja wa Kanda ya Kinondoni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahara Kayugwa (hayupo pichani) wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko wa pensheni wa PPF iliyokuwa na lengo la kuwaelimisha waajiri kuhusiana na huduma mbalimbali za PPF ikiwemo huduma mpya ya PPF Taarifa App.
Mgeni
Rasmi Prof Betria Mapunda akiwa katika picha ya Pamoja na Waajiri
pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF leo katika Semina
iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika Katika Ukumbi wa
Seascape Hotel Mbezi Beach Jijini Dar.Picha zote Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
No comments:
Post a Comment