HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 12, 2014

MOTO WAUKUMBA TENA MSIKITI WA MTAMBANI,KINONDONI JIJINI DAR LEO

IKIWA ni tofauti ya  siku moja kufanana  kwa tarehe ya janga la moto leo Septemba  12 msikiti  wa  Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es Saam uliungua kwa mara ya pilia ambapo moto wa kwanza ulizuka Agosti 13 mwaka huu   na kusababisha mtafaruku kwa waumini wake pamoja na waislamu wengine kwa  ujumla.
Msikiti huo ambao kwa mara ya kwanza uliuungua katika ghorofa yake ya juu na kuteketeza  eneo kubwa ambalo hadi sasa bado halijanza kufanyiwa  ukarabati.

Ghafla jana ulizuka moto ambao unasadikika  ulianza saa sita na nusu mchana  jana katika moja ya chumba ambacho wanafunzi wa kidato cha nne  wa kike wamekuwa wakipiga kambi ya kujisomea ikiwa ni katika maandalizi ya kukabiliana na mtiwao wa taifa  utakaofanyika  baadaye mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika eneo la msikiti huo Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kanda ya Kinondoni Camilius Wambura alisema  hadi wanafika eneo la tukio chanzo bado hakijafahamika.

Aidha Wambura   aliongeza kwa kusema kwamba chumba ambacho moto ulianzia ni chumba cha wasichana na magodoro manne yameungua.
“Katika janga la moto uliounguza madarasa  mwezi uliopita Jeshi la Polisi lilinda  timu ambayo ilikuwa ikichunguza chanzo cha moto huo hivyo na sasa timu hiyohiyo itaendele na uchunguzi wake kwa kuunganisha matukio haya mawili” alisema Wambura.
Wakizungumza bila ya kutajwa majina yao kina mama wa msikitini hapo wao walisema  kwamba “ sisi tulikuwa msikitini tunasoma qurani wakati tukivuta muda was ala ya Ijumaa ndipo tuikasikia sauti za moto moto na kuona upande wa wanaume wakikimbia huku na kule kwa taharuki hivyo chanzo hasa cha moto sisi hatukijui.

Licha ya kuwa hili ni tukio la pili la moto kutokea kwenye msikiti wetu ndazi ya siku chache tu huenda ikawa labda ni mwezi tu tangu moto wa awali ulipotokea imani yetu ya dini ya kiislamu inatukataza dhana hivyo wala hatumdhanii mtu yeyote  kusababisha moto huu.

“Mwenyeezi mungu  ndiye anaejua  kila kitu hivyo tuna imani kubwa kwamba iko siku atafichua  ukweli wa chanzo ama sababu za  moto huu ila jambo la kushukuru ni kwamba moto huu umetokea muda ambao kila mtu ananguvu za kuuzima hilo ni jambo la kushukuru  kwani laiti kama ungetoea nyakati za usiku hali ingekuwa mbaya” walisema kina mama hao.

Waumini wa msikiti huo walifanikiwa kuuzima moto huo na kusali swala ya Ijumaa kama kawaida.Agosti 13  mwaka huu msikiti wa Mtambani uliungua moto .


Sehemu ya Waokowaji wakiendelea kufanya juhudi za kuuzima moto huo.Picha na KajunasonBlog.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad