Katiba Tawala wa Wilaya ya Moshi mjini,Remida Ibrahim(wa pili kulia) akicheza kuashilia uzinduzi wa fainali za mashindano ya Pool Taifa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” yanayofanyika katika Ukumbi wa Kuringe Mkoani Kilimanjaro.Kutoka kushoto ni Katibu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga,Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Makamu Mwenyekiti wa TAPA, Fred Mushi.
Baadhi ya Wachezaji wa Pool wakiwa na zawadi mbalimbali wakielekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi kutoa kwa wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile wanachofadhiliwa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wa ufungunguzi wa mashindano ya Pool Kitaifa yanayofanyika Mkoani humo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”.
Baadhi ya wachezaji wa Pool wakitoa zawadi za vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile wanachofadhiliwa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wa ufungunguzi wa mashindano ya Pool Kitaifa yanayofanyika Mkoani humo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”.
WACHEZAJI wa mchezo wa pool nchini wametakiwa kutumia mchezo huo kama sehemu ya ajira kwao na pia sehemu ya kukukutana na kupeana mawazo ya kuinuana kimaisha.
Hayo yamesemwa jana na Katiba Tawala wa Wilaya ya Moshi mjini,Remida Ibrahim wakati alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Ibrahim Msengi katika ufunguzi wa fainali za taifa za mashindano ya ‘Safari Lager National Pool Championship 2014’, zinazofanyikia kwenye ukumbi wa Kuringe mkoani hapa.
Ibrahim alisema mchezo huo kwa sasa ni ajira kwa wanaoucheza, hivyo ni vema wachezaji wakautumia vizuri kwa ajili ya kuwainua kimaisha badala ya kuutumia kwa masuala ambayo hayana faida katika maisha yao.
“Nitumie nafasi hii kuwashukuru wadhamini wa mchezo huu bia ya Safari lager kutokana na kwamba umeongeza ajira kwa vijana, hivyo wachezaji niwasihi tumieni mchezo wa pool kuweza kuinua maisha yenu na pia mnapokutana katika mashindano kama hayo tumieni nafasi hii kushauriana masuala ya msingi ya kuwainua kimaisha,”alisema Ibrahim.
Naye menaja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo aliwataka wachezaji wa timu zote zinazoshiriki fainali hizo kucheza kwa utulivu hadi mwisho wa fainalio hizo.
Shelukindo alisema haitakuwa jambola busara endapo fainali hizo zitamalizika huku wakiacha gumzo la vitendo ambazo si vya kiungwana. “Kwanza niwape pole kwa uchovu wa safari ndefu mlikotoka kwenye mikoa yenu kwa ajili ya kufika hapa kushiriki fainali hizi lakini niwombe tucheza kwa amani bila ya kufanya jambo lolote la kuashiria vurugu na tukitoka hapa tuache simulizi nzuri mkoani hapa,”alisema Shelukindo.
Kabla ya fainali hizo kufunguliwa rasmi wachezaji na viongozi wa chama cha mchezo huo taifa (TAPA) pamoja na meneja wa bia ya Safari Lager, Osacr Shaelukindo walitembelea wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Mawenzi na kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo unga, juice, sabuni , biscut, mafuta ya kupaka na pesa taslim.
Timu zinazoshiriki fainali hizo na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Blue Leaf (Lindi), Bilele (Kagera), Mpo Afrika (Temeke), Mashujaa (Ilala), Topland (Kinondoni), Yakwetu (Pwani), Billiard (Mwanza) na New Stend (Shinyanga).
Nyingine ni Delux (Dodoma),Black Point (Mbeya), Ngarenaro (Arusha), Nginja Master (Iringa), Corner Kasara (Manyara), Absom (Tanga), Anatory (Morogoro), Tiptop (Tabora) na wenyeji Mboya (Kilimanjaro).
No comments:
Post a Comment