Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kivuko kipya cha MV Tegemeo kitakachotoa huduma kati ya Kahunda hadi kisiwa cha Maisome katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza. Wengine walioshikilia utepe ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli , Mbunge wa Buchosa Dkt Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Ujenzi.
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akibonyeza kitufe
kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko hicho kipya cha MV Tegemeo.
Kivuko kipya na chakisasa cha MV Tegemeo kama kinavyoonekana, kimetengenezwa kama mfano wa Meli kutokana na huduma zake.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha Makamu wa Rais Dkt.
Mohamed Gharib Bilal jinsi kivuko kipya cha MV Tegemeo kitakavyofanya
kazi.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Marceline Magesa
akimuonesha Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal baadhi
ya sehemu ndani ya Kivuko hicho kipya.
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa pamoja na Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutoka kukagua sehemu ya
kuendeshea kivuko hicho
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa pamoja na Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia ngoma iliyokuwa ikichezwa
ndani ya kivuko hicho kipya.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kushoto akifurahia jambo na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Dkt Charles Tizeba kabla ya uzinduzi wa Kivuko cha MV Tegemeo.
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kulia akizungumza na
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiwa njiani ndani ya
Kivuko cha MV Misungwi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za ufunguzi
wa kivuko kipya cha MV Tegemeo.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia akimsikiliza Mbunge wa Buchosa
na Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba wakati wa
Uzinduzi.
No comments:
Post a Comment