HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 28, 2014

Ikulu yang’ara SHIMIWI Morogoro

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa kwenye maandamano siku ya ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI taifa yanayoendelea mjini Morogoro.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Ikulu wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI taifa yanayoendelea mjini Morogoro.
Yameanza vema mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa kuendeleza ushindi na kung’ara katika mashindano hayo yanayoendelea mjini Morogoro.
Mfungaji mahiri wa magoli wa timu ya mpira wa pete Ikulu aliyecheza nafasi ya (G.S) Monica Kassy akiwania mpira dhidi ya wapinzani wao RAS Morogoro wakati wa mechi ya ufunguzi ambapo Ikulu walishinda kwa magoli 62 kwa11 dhidi ya wapinzani wao.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Ikulu wakifuatilia mchezo wa mpira wa pete wanawake kati ya timu yao na wa wapinzani wao RAS Morogoro. (Picha zote na Eleuteri Mangi MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad