HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 25, 2014

MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI YAENDELEA VIWANJA VYA MASHUJAA MJINI DODOMA

Na Andrew Chale,Dodoma.

MAONYESHO ya wafanyabiashara kipindi cha Bunge Maalum la Katiba yanaendelea kwa kasi mjini hapa na kuwakutanisha wajasiriamali zaidi ya 100 katika viwanja vya Mashujaa.

Akizungumza katika maonyesho hayo,Mwenyekiti wa wajasiriamali, Dokta Haruna Kifimbo, alisema lengo kuu la maonyesho hayo ni kutoa fursa kwao kuuza na kunadi bidhaa zao kwa watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Bunge hilo.

“Mpaka sasa tuna wajasiriamali 100, ambao wanaendelea na maonyesho yao kwenye viwanja hivi vya Mashujaa kuanzia Agosti 10 mwaka huu, na maonesho yataendelea mpaka litakapomalizika Bunge la Katiba, hivyo bado tunaendelea kupokea wajasiliamari wengine zaidi,” alisema Dk. Kifimbo.

Alisema kuwa maonyesho hayo yanajumuisha wauzaji wa bidhaa za tiba mbadala, bidhaa za majumbani, kazi za mikono kutoka ndani na bidhaa zingine mbalimbali.

Kifimbo ambaye ni mganga wa tiba mbadala alisema maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi Agosti 21, mwaka huu, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, na kutoa rai kwa wananchi kushiriki.

Lengo ya maonyesho ni kutoa fursa kwakuuza na kunadi bidhaa zao kwa watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Bunge hilo.
Mwenyekiti wa wajasiriamali, Dokta Haruna Kifimbo (Kulia) akipata maelezo ya moja ya banda linaloonyesha na kuuza bidhaa zake za madishi na vifaa vya umeme, kwenye maonesho ya biashara za wajasiriamali yanayoendelea katika viwanja vya Mashujaa, mjini Dodoma.
Baadhi ya wateja wakichagua moja ya bidhaa za dvd na cd zinazouzwa kwenye mabanda hayo.
Baadhi ya wakina mama wakiwa wanaangalia bidhaa mbali mbali zinazouzwa katika mabanda ya wajasiriamali hao yanayoendelea hivi sasa mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad