HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 12, 2014

Ujumbe Muhimu kwa Wanachama, Wadau na wandishi wa Habari wasiokuwa wanachama wa MBPC

Ndugu wanachama, Wadau na wandishi wote wa Habari,

 Kuna ujumbe unaozunguka miongoni mwetu, kwa wandishi wa habari wasiokuwa wanachama  na kwa wadau wetu ukieleza kwamba MBPC imeandaa safari ya wanachama wake kutembelea nchi Jirani ya Malawi. Ujumbe huu unawataja baadhi ya wanachama wa MBPC kuwa ndio waratibu wa Safari hiyo, huku ukiwataka wanachama na wadau kuchangia safari hiyo fedha kiasi cha shilingi 200,000 (Laki mbili) kwa kila mwanachama na mwandishi wa habari yeyote asiyekuwa mwanachama wa MBPC.

Kwa niaba ya uongozi wa MBPC napenda kuwataarifu Wanachama wa MBPC, Wandishi wa Habari wasiokuwa wanachama na wadau wetu kuwa mpango huo hauna utashi wala Baraka za MBPC, hivyo kwa yeyote Atakayejihusisha  na mpango huo atambue kuwa atafanya hivyo kwa dhamana yake mwenyewe na sio ya MBPC.

MBPC inawataka na kuwaonya  wanachama na watu wasiokuwa wanachama walio nyuma ya mpango huo kuacha mara moja kutumia jina la MBPC katika kuratibu mambo yao la sivyo hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.

Uongozi wa MBPC unawataka watu hao kama wanaona mpango huo una kila sababu ya kutumia jina la MBPC wafike ofisini na kufuata taratibu zote ili kupata Baraka za MBPC.

Mwisho naomba kuwaasa wanachama wa MBPC kutojihusisha wala kuupapatikia mpango huo kwani kuna dalili kuwa mwisho wake sio mzuri.

Nawatakieni kila la Heri

Emmanuel Lengwa – KATIBU MBPC.

Asante.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad