Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (wa pili kulia) akipongezana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) Engineer George Mulamula mara baada ya kutiliana saini ya ushirikiano ambapo Tigo itawawezesha washiriki wa teknohama wa DTBi kuendeleza vipaji vyao kupitia mpango maalum wa mafunzo na biashara ambayo itasaidia kukuza ajira nchini kupitia taaluma ya teknohama. Kushoto ni Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Hassan Mshinda.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (kulia) akitiliana saini na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) Eng. George Mulamula kama ishara ya ushirikiano kati ya Tigo na kituo hicho cha biashara ya teknohama DTBi. Wanaoshuhudia kutoka nyuma ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dk. Hassan Mshinda. Tigo itatoa nafasi ya kuwasomesha watanzania 10 katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kila mwaka.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (kushoto) wakimsikiliza kwa makini mmoja wa washiriki wa mpango maalum wa Tigo na DTBi katika kukuza vipaji vya teknohama Bw. Godfrey Magila ambaye ameweza kubuni programu ya kuangalia vipindi vya Bunge kupitia simu za mkononi za kisasa. Tigo pia itatoa fursa za mafunzo kwa vitendo na nafasi za ajira kwa wale ambao wamejikita katika masomo ya Teknohama.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya utiliaji saini kati ya kampuni ya Tigo na kituo cha biashara ya teknohama DTBi. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez na Afisa Mtendaji Mkuu wa DTBi Eng. George Mulamula
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) Engineer George Mulamula akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani)
wakati wa hafla fupi ya utiliaji saini kati ya kampuni ya Tigo na kituo
cha biashara ya teknohama DTBi.
No comments:
Post a Comment