Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unawakaribisha wanachama na wananchi wote kwa ujumla katika banda lake kwenye maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 16 hadi 23/06/2014.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utatoa huduma zifuatazo;-
• Elimu kwa Umma juu ya Huduma za NHIF na CHF/TIKA
• Usajili wa wanachama
• Upimaji wa afya bure kwa wanachama na wananchi wengine na vipimo vitakavyotolewa ni;-
1. Kisukari,
2. Shinikizo la damu,
3. Hali Lishe
4. Saratani ya matiti.
5. Ushauri wa Kitaalam wa namna ya kuepukana na maradhi yasiyoambukiza.
WOTE MNAKARIBISHWA
No comments:
Post a Comment