Baadhi ya wabunge wameitaka serikali kupitia Wizara ya Maji kuunda haraka chombo kitakachosimamia huduma ya Maji vijijini katika mwaka huu wa fedha wa 2014/2015.
Wabunge hao wametoa hoja hizo wakati wakiwasilisha mIchango yao katika bajeti ya Wizara ya Maji ambako wengi wa wachangiaj hao waliona umuhimu wa kuwepo chombo kinachosimamia Maji vijijini na wakatolea mfano wa Mfuko wa Umeme Vijijini (REA).
Wa kwanza kuchangia kuundwa kwa mfuko huo alikuwa ni Mh Jasson Rweikiza wa Bukoba Vijijini (CCM) alisema ipo haja kwa serikali sasa kuunda chombo kitakachosaidia wananchi wanaoishi Vijijini kwani ndio waathirika wakuu wa tatizo la Maji nchini.
Alitaka serikali kupitia wizara ya Maji kuandaa vyanzo maalumu vitakavyoendesha mfuko huo ili wananchi waweze kupata huduma ya Maji safi na Salama kwa wakati. Alitolea mfano wakala wa barabara nchini (TANROAD) jinsi inavyosaidia serikali katika ujenzi wa barabara na mafanikio yake ndani ya kipindi kifupi tangu kuanzishwa.
Nae mbunge wa Lushoto (CCM), Mh Henry Shekifu aliitaka serikali kuleta mswada wa uundwaji wa Mfuko wa Maji nchini ili kilio cha wana lushoto na watanzania wengine kipungue.
“Ni muda muafaka sasa kwa serikali yetu kuleta muswada utakaojadiliwa na kupitishwa ili chombo hiki maalum kisaidie kupunguza kero sugu ya watanzania hasa kwenye sekta ya Maji” alisema shekifu.
Nae mbunge wa Singida Kusini Mh Mohamed Misanga alitaka serikali kuu kuisaidia Wizara ya Maji ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa urahisi na kwa wakati kwa kutoa fedha zaidi pindi zinapoidhinishwa na bunge.
Waziri wa Maji Mh Prof Jumanne Maghembe na naibu wake Mh Amos Makala wakifatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wa kipindi cha michango mbalimbali ya wabunge wakati wakipitisha bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2014/2015.
No comments:
Post a Comment