Siku
moja katika pita pita za Mdau Juma Mtanda,alikatiza barabara ya
Sabasaba Mkoani Morogoro na kufanikiwa kuzinasa taswira hizi za Mbuzi wakila majani katikati ya barabara na kusababisha magari na vyombo
vingine vinavyotumia barabara hiyo vikiwa na upole usiotegemewa kama
inavyoonekana pichani hapa.kwa mujibu wa baadhi ya wapita njia hiyo
wameeleza kwamba mbuzi hao wenye uwezo wa kipekee wa ulaji wa majani katikati ya lami ambao wako makundi kwa makundi,pamoja na kwamba
halmashauri ya Manispaa hiyo ya Morogoro imeipiga mikwara mifugo hiyo pamoja na wamiliki wake,lakini wenyewe hawajali wala nini na ndio kwaanza wanaendelea kupiga misele.
Mbuzi hawa hawaogopi cha nini wala nini,si unaona hapa jinsi walivyoizunguka hii baiskeli.
No comments:
Post a Comment