Imeelezwa kuwa upungufu wa rasilimali za Maji nchini ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya Maji na kusababisha maeneo mengi kukubwa na uhaba wa Maji. Miongoni mwa sababu za upungufu huo ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, uvamizi katika vyanzo vya Maji kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, uchafuzi wa vyanzo vya Maji na matumizi holela ya Maji.
Katika hotuba yake ya bajeti kwa wizara ya Maji Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe alisema athari ya moja kwa moja kwa wananchi ni ukame wa muda mrefu unaosababishwa na kutotabirika kwa urahisi majira ya Mwaka na mtawanyiko wa Mvua.alisema matukio yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi yanaathiri vyanzo vya Maji pamoja na miundo mbinu yake.
Alisema wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo kuwekeza katika ujenzi na uendelezaji wa vyanzo vya Maji na kuhifadhi maeneo oevu. Hatua hizi zinalenga kuboresha upatikanaji wa Maji kwa kipindi chote cha mwaka .
“Wizara imeandaa mipango shirikishi ya uendelezaji na usimamizi wa rsilimali za Maji kwa Bodi za Maji za mabonde kama njia mojawapo ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi” alisema Prof Maghembe.
”Kupitia jukwaa la majadiliano ya athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta ya Maji, wizara itashirikiana na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali pamoja na wadau wengine katika utambuzi wa mbinu za kukabiliana na athari hizo kupitia taarifa za shughuli zinazotekelezwa na wadau hao na tafiti mbalimbali zinazofanywa na wadau hao na tafiti mbalimbali zinazofanyika nchini kuhusiana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye sekta ya Maji”aliongeza Prof Maghembe.
Uharibifu wa mazingira kandokando ya Mto Mgeta, uliopo Morogoro ambao ni chanzo kimojawapo cha Mto Ruvu.
No comments:
Post a Comment