Kampuni ya Ericsson (NASDAQ: ERIC), inayoongoza katika teknolojia na huduma ya mawasiliano duniani leo inatoa taarifa ya utafiti inayohusu mapinduzi ya data inayo husiana na ongezeko la watumiaji wa simu katika ukanda wa Sahara.
Utafiti wa Sub-Saharan Africa Ericsson Mobility Report inaonesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2014 watumiaji wa simu waliweza kufikiwa na kiasi cha 76,000 TB (terabyte) cha taarifa kwa mwezi ambapo kiasi hiko kimeonekana kuwa ni mara mbili ya kiasi cha taarifa zilizo wafikia wateja kwa mwaka 2013 ambapo ilikuwa kiasi cha 37,500 TB kwa mwezi. Pia kwa mwaka 2015 idadi hiyo ya taarifa inakadiliwa kuongezeka marambili kwa watumiaji wake na wateja na kufikia 147,000 TB kwa mwezi.
Kuenea kwa mitandao ya kijamii na taarifa kwa njia za video kupitia teknolojia ya Apps katika simu zenye gharama nafuu kumepelekea ongezeko hilo la taarifa kwa wateja pia wateja kutoka nchi kama Nigeria, Afrika Kusini na Kenya wameongeza matumizi ya simu kupata vituo vya televisheni pamoja na huduma nyingine vya vyombo vya habari.
Meneja wa Ukanda wa Sahara kampuni ya Erricsson, Bw. Fredrik Jejdling, alieleza “kwa sasa nchi za ukanda wa Sahara zinaendelea kukua katika matumizi ya teknolojia ya simu za digitali kwa wateja, mitandao ya simu pamoja na vyombo vya habari, ambapo jamii inaamka na kuanza kuangazia zaidi matumizi ya teknolojia ya 3G na 4G. Kama tulivyoona idadi ya watumiaji inavyozidi kupanda katika vipindi vifupi vya mwaka lakini hapo nyuma kipindi cha mwaka mmoja uliopita ongezeko la matumizi ya digitali yaliongezeka zaidi ya 100% ambapo ilipelekea tutazame upya matarajio yetu katika kipindi kijacho.”
Taarifa ya utafiti uliofanywa unaonesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo simu za sauti katika Ukanda wa jangwa la sahara zitaongezeka mara 20 ambapo itakuwa ni mara mbili ya ilivyo tarajiwa hapo awali. Pia utafiti huo unaonesha kuwa kufikia mwaka 2019, 75% wateja watakua wameunganishwa katika matumizi ya interneti yenye taknolojia ya 3G au 4G.
Makadilio ya ukuaji huu yametokana na kuingia kwa aina mbalimbali za simu za kidigitali zinazouzwa chini ya TSH 80,000 ambapo inapelekea kukua kwa kasi ya matumizi ya teknolojia ya 3G na 4G. Taarifa za mwaka 2014 inaonesha kuwa katika miaka mitatu ijayo teknolojia ya 3G ndio itakayo ongoza kwa matumizi katika maeneo ya kanda ya jangwa laSahara.
“Kuibuka kwa simu za gharama nafuu zitapelekea ongezeko la matumizi ya simu zenye uwezo wa intaneti hasa kwa watu wa tabaka la kati waishio mijini pamoja na wafanya biashara waishio vijijini. Huduma za kifedha kupitia simu za mkononi zimeonekana kuwa chachu ya ongezeko hilo pia wakulima wengi wameipenda huduma hiyo inayotolewa na makampuni mbalimbali ya mawasiliano, vile vile vijana wengi upenda kuangalia video mbali mbali kupitia simu za mkononi” aliongezea Bw Jejdling
Kampuni ya Ericsson imefany utafiti katika mitandao 100 tofauti ambapo matarajio hayo na matokeo yamepatikana kwa kushirikiana na kitengo cha Ericsson kinacho shughulikia wateja, idadi ya watu, maendeleo ya kiuchumi pamoja na kampuni inayo miliki taarifa. Ericsson ni kampuni inayo jiusisha na masuala ya usimamizi wa huduma, inyojenga na kuboresha uwezo wa mitandao ya simu katika kufikia wateja katika nchi za Afrika zilizoko katika Ukanda wa jangwa la Sahara na kimataifa.
No comments:
Post a Comment