HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 1, 2014

Castle Lager Perfect Six yanoga kuelekea fainali za Kanda

Timu nne za soka za kanda ya mashariki zimefanikiwa kuvuka na kutinga hatua ya ligi ndogo ya mashindano ya Castle Lager Perfect Six kwa mikoa ya Morogoro na Dodoma.

Katika michezo ya hatua ya mchujo ikirishikisha timu nane za mikoa hiyo, kwa upande wa Morogoro timu za Mzinga FC na Ndezi FC zenyewe zilikata mapema tiketi ya kucheza ligi hiyo huku kwa Dodoma ikiwa ni Schalke 04 FC pamoja na Market FC.

Schalke 04 na Market FC zilikata tiketi juzi kwa kushika nafasi ya kwanza na pili katika uwanja wa Central msikiti wa Gadaff mjini Dodoma baada ya kuvuka katika hatua ya mchujo wakati Ndezi FC na Mzinga FC zikifanya hivyo katika michezo iliyofanyika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.

Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo waandaaji wa Castle Lager Perfect Six alisema kuwa baada ya kumalizika kwa hatua ya mchujo kwa michezo iliyofanyika Morogoro na Dodoma inayounda kanda ya mashariki na kupata timu nne, timu hizo zitacheza ligi ndogo ili kupata timu moja itayowakilisha kanda ya mashariki katika mashindano hayo ya taifa jijini Dar es Salaam.

Nshimo alisema kuwa ligi ndogo itafanyika Juni 7 mwaka huu Manispaa ya Morogoro kwa kuzikutanisha washindi wa kwanza wa Dodoma ambazo ni timu za Schalke 04 na Market FC na Ndezi FC na Mzinga FC ili kucheza na kupata mshindi wa kanda ya mashariki atayewakilisha kanda hiyo kwenye mashandano hayo jijini Dar es Salaam.

Alisema shindano la Castle Perfect Six limelenga kuzungumza na wanywaji wa Castle Lager ambao wana shauku ya kucheza mpira wa miguu na kujumuika pamoja. 

Nshimo alisema kuwa mechi zilizochezwa wikendi hii zimeonyesha jinsi gani Watanzania wana mwamko na shauku kubwa ya kushiriki mashindano kutokana na watu kujitokeza kwa wingi maeneo mbalimbali ambapo yalifanyika mashindano hayo ya kwanza.

Vilevile wikendi hii yalifanyika mashindano hayo kwenye mkoa wa Dar es salaam kwenye viwanja vya Barafu Mburahati, uwanja wa Garden uliopo Kinondoni, Bulyaga Temeke katika hatua za awali za kupata wawakilishi wa Kanda hiyo watakaocheza fainali za taifa. Mashindano yanaendelea pia kwenye mikoa ya Mwanza na Musoma katika hatua ya mwanzo kupata wawakilishi wa kanda ya Ziwa.

Mechi zilizochezwa wikendi hii ilikuwa ni awamu ya kwanza ya mashindano hayo ambapo timu zitakazofuzu hatua hiyo ya mikoa zitachuana katika ngazi ya kanda na hatimaye taifa. Washindi wa fainali za taifa watajipatia fursa ya kipekee kwenda kutembelea jiji la Barcelona huko Hispania na kuiona timu ya Barcelona ikicheza na pia wataweza kujionea mambo mbalimbali ya kihistoria katika uwanja wa Camp Nou.
Mchezaji wa timu ya Matema,Hafidh Mohammed (kulia) akipiga hesabu za kumtoka mchezaji wa IP Sports Club, Hamis Daudi katika mashindano ya Castle Lager Perfect Six kwenye viwanja vya Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.Matema ilishinda 2-0.
Mchezaji wa timu ya IP Sports Club,Hassan Chidigo (kushoto) akijaribu kufunga katika gori la Matema,katika mashindano ya Perfect Six kwenye viwanja vya Garden kinondoni jijini Dar es Salaam jana.Matema ilishinda 2-0.
Kipa wa timu ya Matema,Wahabi Mkambe (kulia) akimpiga chenga mchezaji wa IP Sports Club,Jaffary Madega katika mashindano ya Castle Lager Perfect Six kwenye viwanja vya Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.Matema ilishinda 2-0.
Mchezaji wa timu ya Matema,Hafidh Mohammed (kulia) akipiga chenga mchezaji wa IP Sports Club,Hamis Daudi katika mashindano ya Castle Lager Perfect Six kwenye viwanja vya Garden kinondoni jijini Dar es Salaam jana.Matema ilishinda 2-0.
Mchezaji wa Timu ya, Pile FC, Ukwama Bonny katikati akiwatoka wachezaji wa timu ya Mwangaza, wakati wa Mchezo wa Fainali katika Bonanza Castle Lager Perfect Six uliofanyika kwenye Uwania wa Buliyaga Temeke Dar es Salaam ilishinda kwa penati, 6. 5.
Kipa wa timu ya Rafael Abuu Mauri (kushoto) akijaribu kumtoka mchezaji wa Saigon, Ally Said zote za Mburahati katika bonanza la ‘Castle Lager Perfect Six’ lililofanyika mwishoni mwa wiki katika kiwanja, Mburahati jijini Dar es Salaam ambapo kwa washindi wa jumla watapata fursa ya kwenda katika jiji la Barcelona, Hispania kuishuhudia timu ya Barcelona. Saigon ilishinda 4-1.
Mchezaji wa timu Saigon, Habib Iman akijaribu kumfunga kipa wa timu ya Rafael Abuu Mauri zote za Mburahati katika bonanza la Castle Parfect Six lililofanyika mwishoni mwa wiki katika kiwanja, Mburahati jijini Dar es Salaam ambapo kwa washindi wa jumla watapata fursa ya kwenda katika jiji la Barcelona, Hispania kuishuhudia timu ya Barcelona. Saigon ilishinda 4-1.
Wachezaji wa timu ya Rafael, Habib Iman (kushoto) na Omary Nchimbi wa Sigon zote za Mburahati wakikabana katika bonanza la Castle Lager Perfect Six lililofanyika mwishoni mwa wiki katika kiwanja, Mburahati jijini Dar es Salaam ambapo kwa washindi wa jumla watapata fursa ya kwenda katika jiji la Barcelona, Hispania kuishuhudia timu ya Barcelona. Saigon ilishinda 4-1.
Mchezaji wa timu ya Barcelona, Ally Rajabu (kushoto) akijaribu kumtoka mchezaji wa Saigon, Ally Said zote za Mburahati katika bonanza la Castle Lager Perfect Six lililofanyika mwishoni mwa wiki katika kiwanja, Mburahati jijini Dar es Salaam ambapo kwa washindi wa jumla watapata fursa ya kwenda katika jiji la Barcelona, Hispania kuishuhudia timu ya Barcelona. Saigon ilishinda 3-1.
Mchezaji wa timu ya Market FC, Kamal Omary akichuana Mgaya Daud wa timu ya Kisimpite FC kushoto wakati wa michezo ya kusaka timu mbili za mkoa wa Dodoma zitazoshindana na nyingine mbili za Morogoro ili kucheza ligi ndogo na kupata timu moja itayowakilisha mashindano ya Castle Lager Perfect Six kutoka kanda ya katika michezo iliyofanyika kwenye uwanja wa Centel mjini Dodoma juzi ambapo katika mchezo Martet FC ilishinda bao 2-1.
Mchezaji wa timu ya Market FC, Medi Mwanyemba kushoto akizongwa na mchezaji wa Kisimpite Mgaya Daud kulia wa timu ya Kisimpite FC kushoto wakati wa michezo ya kusaka timu mbili za mkoa wa Dodoma zitazoshindana na nyingine mbili za Morogoro ili kucheza ligi ndogo na kupata timu moja itayowakilisha mashindano ya Castle Lager Perfect Six kutoka kanda ya katika michezo iliyofanyika kwenye uwanja wa centel msikiti wa Gadaff mjini Dodoma juzi ambapo katika mchezo Market FC ilishinda bao 2-1.
Ramadhan Chinja wa timu ya Manzese kulis akipiga krosi dhidi ya Ally Maulid kulia wa Santos wakati wa michezo ya kusaka timu mbili za mkoa wa Dodoma zitazoshindana na nyingine mbili za Morogoro ili kucheza ligi ndogo na kupata timu moja itayowakilisha mashindano ya Castle Lager Perfect Six kutoka kanda ya Kati. Mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa Centel mjini Dodoma juzi ambapo katika mchezo Manzese iliibuka na ushindi wa bao 3-1.
Ramadhan Chinja wa timu ya Manzese (katikati) akipiga mpira huku mbele ya wachezaji wa Santos Rashid Seif kushoto na Athaman Lukinda kulia wakati wa michezo ya kusaka timu mbili za mkoa wa Dodoma zitazoshindana na nyingine mbili za Morogoro ili kucheza ligi ndogo na kupata timu moja itayowakilisha mashindano ya Castle Lager Perfect Six kutoka kanda ya kati. Michezo hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa Centel mjini Dodoma juzi ambapo katika mchezo Manzese iliibuka na ushindi wa bao 3-1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad