HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 10, 2014

CASTLE Lager mdhamini rasmi matangazo ya luninga Kombe la Dunia

Mwandishi wa habari za michezo Ezra Kaaya (kushoto) akiubusu mpira wa Brazuca ambao utatumika kama mpira rasmi wa Kombe la dunia baada ya kukabidhiwa mpira huo kama zawadi na Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Buttallah kwenye hafla ya kutangaza Castle Lager kama mdhamini rasmi wa matangazo ya luninga ya Kombe la Dunia kupitia SuperSport hapa nchini na Afrika nzima. Katikati ni Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo.

Katika kuendeleza ushirikiano wake na chapa zinazoongoza duniani pamoja na matukio makubwa ya michezo kimataifa, mwaka huu Castle Lager itakuwa itakuwa mdhamini wa matangazo ya luninga ya Kombe la Soka la Dunia kupitia SuperSport, idhaa ya michezo inayoongoza barani Arika.

Udhamini huu unamaanisha kwamba Castle Lager itahakikisha wapenzi wa sokana wanywaji wa Castle Lager barani Afrika wanafurahia matangazo bora ya shindano kubwa zaidi la soka duniani ambalo litaanza mwezi huu nchini Brazil.

“Ikiwa ni chapa ambayo inafahamika kwa kujihusisha na mpira wa miguu barani Afrika, tumeona ni vizuri kushirikana na SuperSport, idhaa ya michezo inayoongoza barani ili kuwaletea wanywaji wa Castle Lager na wapenzi wa soka matangazo ya Kombe la Dunia moja kwa moja kutoka Brazil,” alisema Fimbo Buttallah, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania.

Vilevile, wanyawji wa Castle Lager na mashabiki wa soka wanatufaika kupitia promosheni mbalimbali ambazo zitawapatia fursa ya kushinda safari kwenda Camp Nou huko Barcelona nchini Hispania nyumbani kwa timu ya FC Barcelona na kukutana na baadhi ya wachezaji wa FC Barcelona ambao watacheza kwenye Kombe la Dunia.

“Mara zote Castle Lager hujitahidi kuwapa wanywaji wake burudani zenye ubora wa kimataifa na hii ni njia mojawapo ya kuwashukuru wanywaji wa Castle Lager kwa kutuunga mkono na wakati huo huo tukitumia manufaa ya ushirikiano wetu na FC Barcelona kwa kuwapa nafasi ya kipekee kabisa wanywaji wa Castle Lager kuwaona wachezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani ambao wanaichezea FC Barcelona, mojawapo ya klabu kubwa zaidi duniani,” amesema.

“Wakati Kombe la Soka la Dunia likikaribia, wanywaji wa Castle Lager wajitayarishe kwa promosheni kabambe mbalimbali kutoka kwa bia yao waipendayo kwa ajili yao kushiriki na kujipatia nafasi ya kukutana na baadhi ya wachezaji soka wawapendao,” alisema Kabula Nshimo, Meneja wa Bia ya Castle Lager.

Ni dhahiri kwamba Castle Lager ni mdau mkubwa wa soka barani Afrika kwa miaka mingi, bia hii imejikita katika kudhamini mchezo huu maarufu zaidi duniani katika ngazi mbalimbali,” Nshimo alisema.

Castle Lager imekuwa ikifahamika sio tu kwa kuwa bia inayoongoza barani Afrika lakini pia ikiwa ni chapa ambayo huanzisha ubia na chapa nyingine zinazoongoza kwa ubora au matukio makubwa zaidi duniani. Mwaka jana Castle Lager ilisaini mkataba wa ushirikiano kuwa bia rasmi ya FC Barcelona barani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad