Hali ya utupaji taka kiholela imekithiri katika maeneo mbali mbali ndani ya jiji la Mbeya,Kamera ya Mtaa kwa Mtaa Blog kupitia kwa Kamera mani wake Machachari Bw. Fadhil Atick imezama katika maeneo mbali mbali ndani ya jiji hilo na kufanikiwa kutuletea taswira hizi za hali ilivyo hivi sasa katika maeneo mbali mbali ya Jiji hilo.
Hapa ni mtaani kabisa ambapo ni njia kubwa tu na pia kuna makazi ya watu,lakini ndio imekuwa kama Dampo maalum la kuhifadhia taka hizo.
Pamoja na kwamba hapa kuliwekwa kibanda cha kuhifandhia taka hizo,na kibanda hicho kinaonekana kujaa na mpaka taka zingine kujitokeza kwa nje.lakini hakuna utaratibu wowote unaoendelea mpaka leo hii.sasa tunashindwa kufahamu,kwamba wenye jukumu la kufanya hivi wamejisahau au ndio mtindo wao wa ufanisi wa kazi.
Jamani oneni wenyewe hali hii,yaani jiji limekuwa kama halina watumishi vile au wakazi wa maeneo husika.
Hapa ni nje ya Shule ya Msingi Maanga,nako mambo ni kama inavyoonekana.
No comments:
Post a Comment