Brass band ikiongoza maandamano ya wanadipolomasia wa nchi za Afrika, watumishi wa Serikali ya Tanzania, wanafunzi na wageni wengine waalikwa kwenda Viwanja vya Karimjee kuadhimisha Siku ya Afrika.
|
Wanafunzi wakiwa wamebeba bendera mbalimbali za nchi za Afrika na ile ya Umoja wa Afrika wakiwa katika maandamano kuelekea Viwanja vya Karimjee.
|
Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Afrika
|
Waheshimiwa Mabalozi wakiendelea na maandamano
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) aliyevaa suti ya rangi ya kijivu akipokea maandamno katika Viwanja vya Karimjee
|
Burudani ya ngoma katika Viwanja vya Karimjee kusherehekea Siku ya Afrika
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt Mahadhi Juma Maalim akiwahutubia watu waliohudhuria sherehe za Siku ya Afrika. Naibu Waziri alipongeza kaulimbiu ya maadhimisho hayo ambayo ni Kilimo na Usalama wa Chakula. Alisema usalama wa Chakula ni changamoto ambayo lazima nchi za Afrika zichukuwe juhudi za pamoja kukabiliana nayo
|
Wanadiplomasia na wananchi wengine wakimsikiliza Naibu Waziri.
|
Balozi wa Kenya akichangia mada Kilimo na Usalama wa Chakula.
|
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt. Yamungu Kayandabila naye akitoa neno wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika
|
Balozi Sweden nchini Tanzania alipata fursa pia ya kuchangia mada katika maadhimisho hayo
|
Picha ya pamoja ya Mabalozi na Mabalozi wastaafu mara baada ya sherehe za kuadhimisha Siku ya Afrika kukamilika
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akihojiwa na wana habari
|
Picha ya pamoja kati ya Dkt. Maalim na Wanadipolomasia.
|
No comments:
Post a Comment